Jumatatu , 20th Jun , 2022

Hii ndiyo maana halisi ya elimu haina mwisho, Baba mmoja wa miaka 32 Joel Majok raia wa Sudan amezua gumzo baada ya kurudia kusoma darasa la tatu ambapo kwa sasa anasoma shule moja na mwanaye wa miaka 8.

Picha ya mzazi huyo akiwa na mtoto wake

Unaambiwa baba huyo amekataa kurudia darasa la 7 na kuchagua darasa la 3 kwa lengo la kujifunza lugha za msingi kama kiswahili na kiingereza kwa sababu hazijui lugha hizo.

Pia ameongeza kusema amerudia kusoma ili kuwa na maisha mazuri kwake na familia yake.

Chanzo : Tuko News

Zaidi tazama video ya Dokii akizungumzia kauli ya Lulu Diva kuchanganya penzi la Rich Mavoko na Boss wake.