
Picha ya Ayanna Williams aliyekuwa na kucha ndefu zaidi duniani
Ayanna Williams amesema ameamua kukata kucha hizo kwa sababu amezichoka na anataka kuwa na maisha mapya na sasa ndio muda muafaka wa kukata kucha hizo japo anajua kabisa atazikumbuka sana.
"Nipo tayari kwa maisha mapya najua nitazikumbuka sana ila ni muda wa kwenda sasa na nilikuwa nimezichoka, niwe na kucha au nisiwe nazo nitabaki kuwa Malkia kwa sababu kucha hazinitengenezi mimi japo mimi ndio nazitengeneza, nimefurahi kuzikata na ninatarajia mwanzo mpya" ameeleza Ayanna Williams
Kulingana na rekodi ya 'Guinness World Record' iinasema Ayanna Willims alivunja rekodi ya kuwa binaadam mwenye kucha ndefu zaidi mwaka 2017, ambapo kucha zake zina futi 19 na inamchukua saa 20 kuzisafisha pamoja na chupa mbili za dawa.