Alhamisi , 27th Mei , 2021

Chuo Kikuu cha Howard cha nchini Marekani kimetangaza kubadilisha jina la kitivo cha Sanaa chuoni hapo na kupewa jina la ‘Chadwick A. Boseman College of Fine Arts’.

Pichani marehemu Chadwick Boseman

ikiwa hili ni jina la muigizaji maarufu wa filamu ya Black Panther aliyefariki mwezi Agosti, 2020 kwa matatizo ya saratani ya utumbo.

Baada ya habari kutangazwa na Chuo, muda mfupi baadae kuliandikwa taarifa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wa marehemu Boseman ikiwakaribisha wanafunzi Chuoni hapo.

Ujumbe wa Boseman wa Twitter

Boseman (43), alihitimu masomo yake  katika chuo hicho mwaka 2000 na alikuwa akichukua Shahada ya Sanaa kwenye masuala ya uongozaji wa filamu.