Zari akiwa na wanawe
Habari hizi ambazo Zari ameshare na mashabiki wake kupitia mtandao wa Instagram, picha inayomuonesha akibatizwa sambamba na maneno 'Its Official', na taarifa hizi zimeanza kuzua mkanganyiko hasa kutokana na hatua ya hivi karibuni ya Zari kuanzisha mahusiano na mwanaume anayejulikana kwa jina Farouk ambaye ni muislam.
Bado madhumuni na msukumo wa Zari kufanya hivi haujajulikana, isipokuwa katika siku za hivi karibuni, mwanamama huyu amebadili kabisa mfumo wake wa maisha na kujiweka karibu na Mungu kwa misingi ya imani ya kikristo.