Jumapili , 12th Jul , 2015

Zahara Muhammad Nakiyanga ametwaa taji la Miss Uganda 2015/2016 na kuvalishwa rasmi taji hilo usiku wa kuamkia leo akiwashinda washiriki wengine 20.

Miss Uganda 2015/2016 Zahara Muhammad Nakiyanga

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 23, alifuatiwa na mshindi wa pili Juliana Nabwowe na watatu Engrid Wanyama.

Nakiyaga alikuwa akichukuliwa kuwa ni miongoni mwa wanaotarajiwa kutwaa taji la 'umiss' na alifanya vyema kuanzia mwanzo na kuwashinda washiriki wengine.