Alhamisi , 30th Jun , 2016

Mmiliki wa studio za Classic Sound Mona Gangstar amezungumza na Enewz baada ya wadau wengi wa muziki kumuona kimya na kuona kama ameishiwa na hawezi tena kusimamisha msanii kama alivyo Belle 9 na Young Killer.

Mona Gangstar na Young Killer

Mona ameeleza juu ya kukatishwa tamaa na wasanii wa Bongo Fleva na huku akisema amejifunza mengi saana ikiwemo namna ya kuishi na msanii inapokuja swala la kazi kwani aliowatoa hapo awali aliwachukulia kama ndugu na kwa njia hiyo alifeli.

Hata hivyo Mona amesema Young Killer hakuondoka vizuri katika lebo yake lakini amegundua kwamba kutokuwa na mikataba yenye wanasheria ndo kulisababisa dogo huyo kuondoka kwa kile alichodai kwamba ni baada ya kuzuzuliwa na umaarufu.

Mbali na hayo Mona amewaambia mashabiki wake kupitia Enews kwamba kwa sasa yupo mbioni kuja na msanii wake Motra ni msanii mkali na amejipanga vizuri kuhakikisha anamtoa na kuja kuwa msanii wa kimataifa kwani huwa anaangalia mbali zaidi.