Alhamisi , 7th Mei , 2015

Staa wa michano wa kike kutoka nchini Kenya, Xtatic amepatwa na msiba mzito baada ya kufiwa na mama yake mzazi ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi ambayo hakuweka wazi.

msanii wa muziki wa nchini Kenya Xtatic akiwa na marehemu mama yake

Msanii huyo pia ameweka taarifa hizo katika kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwafikishia ujumbe mashabiki yake juu ya wakati huo mgumu wa huzuni anaopitia sasa.

Salamu za rambirambi kutoka sehemu mbalimbali zimeendelea kumfikia staa huyo kumpatia faraja na eNewz pia tunamtakia faraja katika kipindi hiki cha maombolezo.