Kanda Bongo Man na Wyre
Kupitia nafasi hii, Wyre anatarajiwa kutoka na kazi ambayo imeboreshwa na ina vionjo vya kisasa kutoka rekodi kama Inde Monie ambayo iliweza kutikisa mawimbi vilivyo katika kipindi cha nyuma.
Wyre amekuwa na rekodi ya kuzitendea haki ngoma za zamani ambazo anazirudia, kitu ambacho kinawapatia mashabiki hamu kubwa zaidi kuona kile atakachofanya kutoka kazi za Kanda Bongoman.