Jumanne , 25th Feb , 2014

Staa wa muziki wa nchini Kenya, Wyre The Love Child ameendelea kupata mashavu makubwa kupitia mafanikio ya muziki wake, na safari hii amechaguliwa kama mjumbe kuingia katika bodi inayoshughulika na mambo ya vijana ya Jiji la Nairobi.

Wyre ameweka wazi taarifa hizi kupitia ukurasa wake wa facebook, na tayari msanii huyu
amekwishaanza kazi yake mara moja, kwa kuwataka vijana wanaoishi katika jiji la Nairobi kutoa mapendekezo ya mambo ambayo wangependa kufanyiwa na serikali yao ili kusaidia katika maendeleo.

Katika nafasi hii Wyre atakuwa miongoni mwa watu wengine mashuhuria ambao watatumia nafasi na umaarufu wao kuhamasisha vijana kujituma na kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.