Jumanne , 4th Mar , 2014

Wyre, msanii wa muziki kutoka Kenya ameweka wazi ndoto zake kubwa za kuongeza wigo wa soko la muziki wa reggae kutoka Afrika Mashariki katika ngazi ya kimataifa, lengo lake kubwa likiwa ni kuona wasanii kutoka ukanda huu wakiwa wanashiriki katika matamasha makubwa ya Kimataifa.

Wyre amesema kuwa, anatamani kusimama kupeperusha bendera ya Kenya katika ngazi ya juu zaidi ya pale ambapo amefikia sasa, huku akiwa na matumaini ya kuingia katika kinyangayiro cha tuzo kubwa kabisa za muziki ikiwepo Grammys.

Wyre ameonyesha moyo na malengo makubwa katika ndoto zake hizi, huku tayari dalili za awali
zikiwa zimeshaonekana baada ya msanii huyu kuingia katika kinyang'anyiro cha kimataifa cha tuzo za muziki za dunia ambapo mchakato wa kupiga kuta unaendelea kwa sasa.

Tags: