Shabiki huyu ameweza kuzigusa hisia za msanii huyu kwa kumwambia kuwa kitu ambacho ameweza kukifanya tangu mwaka huu uanze ni kujipiga picha mpya na kuziweka katika mtandao wa Instagram na kujisahau kabisa katika upande wa muziki.
Wizkid baada ya kuguswa na maoni ya shabiki huyu aliamua kumjibu kuwa licha ya suala zima la kuweka picha instagram, yeye anatengeneza pesa nyingi kuliko ambavyo jamaa huyu anatengeneza katika maisha yake, kitu kilichoonyesha kuwagusa wengi kwa namna tofauti.