Jumatatu , 29th Jan , 2024

Mwanamuziki wa Kenya Willy Paul Msafi anasema hajawahi kuingia kanisani tangu mwaka 2017 kwa sababu kanisa lilimfanyia kitu kibaya lakini siku ya jana ameweza kuingia tena.

Picha ya Willy Paul

“Sijaenda Kanisani tangu 2017 kwa sababu Kanisa lilinifanyia kitu kibaya lakini jana nilihudhuria Ibada ya Kanisa Embakassi na najisikia kufarijika sana. Huu unaenda kuwa mwaka mzuri kwangu coz nimeuanzia kanisani”. ameandika Willy Paul