Jumatatu , 28th Mar , 2022

Usiku wa kuamkia leo nchini Marekani zilitolewa tuzo za filamu za Oscar, na muigizaji Will Smith alizua gumzo katika tuzo hizo baada ya kumpiga kofi mchekeshaji Chris Rock aliyefanya utani kwa kumcheka mkewe Jada Smith kuwa na kipara.

Will Smith alikasirishwa na utani wa Chris dhidi ya mkewe Jada.

 

Chris Rock alifanya mzaha kuhusu kichwa cha Jada Pinkett Smith, kitu ambacho kilipelekea Will Smith kuinuka na kumfuta jukwaani kumpiga kibao.

Jada Smith alishawahi kuweka wazi kuwa anapambana na ugonjwa wa alopecia, ambao husababisha nywele zake kukatika.