Alhamisi , 13th Mei , 2021

Kwanini baadhi ya wanawake hupenda kutoka na wababa ndio lilikuwa swali la leo kwenye show ya DADAZ ya East Africa TV, ambapo mtangazaji Mwanne Othman amesema ni tamaa na uchu wa wazee ndio unaowafanya kutaka wanawake vijana.

Mtangazaji Mwanne Othman

"Mzee anarubuni kwa pesa, simu au vitu vizuri kwa hiyo mtoto anakuwa rahisi kurubuniwa, anaweza akawa mwanafunzi au binti wa ndani lakini tamaa na uchu wa wazee wanaamini hao ndio hawajuzurura sana ili kuwafaidi vizuri, wanasema ni namba D hawataki namba A" Mtangazji Mwanne Othman

Kwa upande wa Bhoke Egina amesema "Sasa hivi imekuwa 'trending' kwamba watoto wanawataka wababa ili kuoneakana vizuri, kusafiri na kutumia simu ya macho matatu kwa hiyo vijana wa life yao hawawezi kuwapa, wanaamini wababa wanaweza kuwapa 'lifestyle' ya aina hiyo"

Aidha dada Najma Paul yeye akasema "Kuna kitu kinaitwa tabia, mimi sitaki ku-base kwa baba au mtoto ila nataka niongee na binti, ukiona mpaka baba anakufuata unatakiwa kuonesha msimamo na kukataa".

DADAZ show ni kila siku ya J3 hadi Ijumaa kuanzia 5:00 Asubuhi mpaka 6:00 Mchana, pia inakuwa live kupitia Facebook na Instagram ya East Africa TV.