Jumanne , 17th Jun , 2014

Wasanii wa muziki wa nchini Kenya, Wangechi, Xstatic, Fena Kitu pamoja na mtayarishaji muziki mahiri Kevin Provoke wameshiriki katika mkutano mkubwa wa siku nne wa jitihada za kupambana na ukatili wa kijinsia duniani, uliofanyika huko London.

Wasanii wa Kenya wakipaform nchini Uingereza

Mkutano huu umewapatia wasanii nafasi ya kukutana na pia kuonesha uwezo wao mbele ya mwigizaji wa kimataifa Angelina Jolie ambaye alikuwa moja ya wenyeviti wa shughuli hii nzima.

Hii imekuwa ni nafasi nyingine ya kipekee kwa Afrika Mashariki kuonyesha uwezo na vipaji kwa upande wa sanaa ya muziki katika ngazi ya kimataifa.