Jumanne , 29th Sep , 2015

Star wa muziki Wangechi kutoka nchini Kenya anatarajiwa kutumbuiza jukwaa moja na kundi la muziki la kimataifa la Morgan Heritage mwishoni mwa wiki huko nchini Kenya.

Staa wa muziki Wangechi kutoka nchini Kenya

Onesho hilo linakuwa ni nafasi nyingine kwa Wangechi kunoa uwezo wake na kupiga hatua kimataifa, ambapo atatumia nafasi hii pia kutambulisha track yake mpya inayokwenda kwa jina Fast Lane, baada ya kumaliza onesho lingine kubwa kuhamasisha amani huko nchini Rwanda.

Kwa umri wake mdogo, Wangechi anakuwa mfano kwa wasanii wengine na vijana kwa ujumla kuendelea kujituma na kujiamini katika kile wanachofanya, akiwa pia ni moja ya wasanii 5 kutoka Kenya ambao wameshiriki katika msimu mpya wa Coke Studio ambalo ni jukwaa lingine kubwa linalotarajia kutangaza muziki wake Afrika.