Ijumaa , 19th Jun , 2015

Rapa Wangechi anaendelea kwa kasi na harakati za kuziba nafasi aliyoiacha katika muziki katika kipindi chote ambacho alikuwa akiuguza majeraha ya ajali, ambapo sasa mbali na kazi nyingine yupo katika matayarisho ya kolabo na msanii Fena Gitu.

Wangechi na Fena Gitu

Wawili hawa wamekuwa pamoja hivi karibuni na kutoa taarifa juu ya kukutana kwao kwa mashabiki kwa njia ya mtandao, wengi wakitarajia kutoka kwa kazi ya aina yake hasa kutokana na ladha tofauti za muziki ambazo wasanii hawa hutumia.

Kwa sasa Wangechi anaendelea kuchana na mawimbi na rekodi yake mpya inayokwenda kwa jina Cardiac Arrest, ikiwa na ujumbe kuhusiana na changamoto na mapito ya ajali mbaya aliyoipata mwishoni mwa mwaka jana.