
Picha ya msanii G Nako Warawara
"Fun Fact kuhusu mimi ni kipindi nacheza mpira jamaa waliniwekea buyu kwenye mpira, walikuwa wanajua napenda sana mpira hivyo walitengeneza jiwe ambalo limesukwa vizuri kama mpira wakaweka kisha nipige, nilivyopiga mguu ulitenguka kwa hiyo tangu siku hiyo wakawa wananiita kigulu huko mtaani kwetu Makao Mapya Arusha" amesema G Nako
G Nako kutokea Kampuni ya Weusi anatajwa kama ni mmoja wa wasanii bora kwenye upande wa vitikiio yaani choras killer na ameshatoa hit songs kibao kama mama yeyoo, gusanisha, arosto na kitonga