
Mchekeshaji Idris Sultan
Mbali na Idris Sultan, washtakiwa wengine ni mfanyabiashara Doctor Ulimwengu (28) mkazi wa Mbezi Beach na Isihaka Mwinyimvua (22) ambaye ni msanii na mkazi wa Gongolamboto.
Idris Sultan ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Luborogwa, ambapo amesema kuwa wakili wake amepata dharura hivyo hatoweza kufika Mahakamani hapo.
Aidha Hakimu Luborogwa alihairisha kesi hiyo hadi Oktoba 29 kwa ajili ya kuendelea, Idris na wenzake wanakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha Maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA).