Alhamisi , 1st Feb , 2018

Msanii wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma ya 'Give it to me', Lulu Diva amedai endapo ndoto yake ya kuwa mwanamuziki isingetimia basi angekuwa mfanyabiashara mkubwa wakuuza vitu vya urembo pamoja na dhahabu.

Lulu Diva ameeleza hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo kutoka East Africa Radio wakati alipoulizwa na mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho Dullah kwamba Lulu Diva asingekuwa mwanamuziki angekuwa nani katika ulimwengu wa sasa. 

"Mimi nisingekuwa nafanya muziki basi ningekuwa mfanyabiashara mkubwa wa kuuza vitu vya urembo ambapo nami pia ningekuwa mrembo pamoja na kuuza vitu vya 'Diamond' (dhahabu)", alisema Lulu Diva.

Mbali na hilo, Lulu Diva amesema zile picha zilizokuwa zinasambaa mtandaoni siku kadhaa zilizopita zikiwa zinamuonesha anapika huku akiwa ameweka miko na vitu vingine vya kupikia chini amedai kwamba halikuwa kusudio lake kufanya hivyo bali alipiga picha bila ya kuangalia mazingira huku akiwataka watu wasimjadili kwa kuwa yeye ni mswahili tosha.

Kwa upande mwingine, mrembo huyo aliweza kutambulisha kibao chake kipya kilichopewa jina la 'amezoea' ndani ya kipindi cha Planet Bongo kutoka East Africa Radio.

Kama hujapata bahati ya kuiona basi itazame hapa chini uone ujio wake mpya wa mwaka 2018.