
AY (Kushoto), Mona (Kulia)
Akiongea kupitia eNewz AY amesema alipotoa hiyo kauli aliitoa kama wazo lakini producer Mona Gangstar amesema yeye anawaza pesa na siyo kuzurura na msanii ili kuongeza ufahamu wake kwa kuwa wasanii hawapendi kulipa hela nzuri studio.
Hata hivyo Mona amemsihi AY kuwashauri wasanii wenzake kulipa vizuri studio na AY pia amemsihi Mon kuacha kufanya kazi na wasanii ambao hawapo tayari kumlipa pesa producer pale anapofanya kazi nzuri.
Tazama hapa video kama walivyowekwa kati kwenye eNewz