
Msanii mkongwe wa bongo fleva, Makamua kutoka wakali kwanza
Makamua amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuona 'game' ya muziki inazidi kupoteza uhalisia wake kwa jamii kutokana na wasanii wengi kukosa maarifa ya utunzi mzuri wa mashairi ili aweze kuuvaa uhusika kamili jambo analoliimba.
“Game ya sasa imekuwa kama ‘buble gum’ kulingana na wanacho ki-introduce ‘upcoming’ ni kitu ambacho kipo ‘so polished’….Kama wamevaa uhusika wa watu wengine na siyo sisi, sisi tulikuwa tulikuwa tuna 'introduce R&B' ya kibongo…Na ndiyo kitu ambacho tunatarajia kukifanya kwa mara nyingine ‘since we gone’ hakuna mtu mwingine amekuja kama vile...'R&B singer' tumewaona wanakuja wamefanya vizuri tunawa-appreciate but' tunarudi tena wenyewe tunavyofanyaga". Alisema Makamua
Pamoja na hayo makamua amesema wingi wa wasanii katika 'industry' umesababisha kuleta changamoto kubwa kwa kuwa kila mmoja anataka kuutangaza muziki wa bongo fleva ili uzidi kufika pande zote za dunia.