Alhamisi , 23rd Oct , 2014

Msanii wa muziki Vanessa Mdee yupo nchini Afrika Kusini kwa ajili ya upigaji picha za Video yake mpya ambayo inatarajiwa kuleta gumzo jingine zito katika tasnia ya muziki kwa upande wa video zenye kiwango mwaka huu.

msanii wa muziki wa bongofleva Vanessa Mdee

Taarifa hizi zimewekwa wazi na Meneja wa msanii huyu, Michele Baldini kutoka Pana Musiq ambayo ndiyo inasimamia kazi za msanii huyu anayefanya vizuri kwa sasa.

Kwa mujibu wa tip ambayo msanii huyu ameitoa kupitia ukurasa wake wa Instagram, mchongo mzima wa video ambayo amekuwa akiishughulikia huko Afrika Kusini kwa sasa ni wa ngoma yake kali kabisa ambayo inafahamika kwa jina 'Hawajui'.