Jumanne , 22nd Dec , 2015

Msanii wa muziki Vanessa Mdee ametoa maneno ya hamasa kwa wasanii wanaochipukia kuwa na malengo, kufanya kazi sana na kufanya maombi, vitu ambavyo binafsi ana amini ndivyo vilivyomsaidia kufikia mafanikio makubwa kabisa ndani na nje ya nchi 2015.

Vanessa Mdee

Vanessa amesema kuwa, ana amini kuwa mwaka 2016 utakuwa mzuri zaidi kutokana na wasanii kuwa wamejipanga zaidi, binafsi kama moja ya wasanii wa kike walio nafasi za juu kwa kufanya vizuri Afrika kwa sasa.