Malaika alionekana kwa mara ya kwanza kama video vixen kwenye video ya Rich Mavoko (Marry Me) mwaka 2012 kwasababu mrembo aliyekuwa amepangwa kwenye video hiyo, Miss IFM wa kipindi hicho hakutokea.
Na Malaika ndio mrembo pekee aliyekuwa eneo la tukio wakati wana-shoot, basi Meneja Maneno akapendekeza Malaika akae kwenye video japo pale alienda kama mtu wa make-up kwenye timu ya Director Adam Juma aliyetayarisha video hiyo. Hii ni kwa mujibu wa Rich Mavoko aliyesimulia katika moja ya mahojiano kwenye kituo cha redio mwaka 2020.
Baada ya muda kigodo Malaika akashiriki kwa mara ya kwanza kama mwimbaji katika wimbo wa Chege unaitwa Uswazi Take Away, uliompa umaarufu mkubwa kisha kuanza kutoa nyimbo zake mwenyewe.