Jumamosi , 5th Apr , 2014

Msanii wa muziki Bwana Misosi, amejikuta akiingia katika changamoto ya kiteknolojia baada ya mtu asiyemfahamu kuingilia ukurasa wake wa Facebook kwa lugha ya kimombo 'kuu-hack', na kuanza kuutumia ukurasa huo kurubuni watu kwa kutumia jina lake.

Bwana Misosi

Msanii wa muziki Bwana Misosi, amejikuta akiingia katika changamoto ya kiteknolojia baada ya mtu asiyemfahamu kuingilia ukurasa wake wa facebook kwa lugha ya kimombo 'kuu-hack', na kuanza kuutumia ukurasa huo kurubuni watu kwa kutumia jina lake.

Misosi amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa baada ya tukio hili kumpata, sasa ameamua kufungua ukurasa mpya katika mtandao wa Facebook, na pia kufahamu kuwa hatahusika na urubuni wowote utakaofanyika na mtu huyu ambaye amemwita mhuni.