Jumanne , 11th Oct , 2022

Mke wa staa wa muziki nchini Tanzania Alikiba, Aileen Alora ameshea ujumbe ulizua gumzo mitandaoni baada ya kuandika kwamba 'Rasmi nipo huru'.

Picha ya pamoja msanii Alikiba na mke wake

Aileen Alora amepost ujumbe huo kwenye 'Insta Story' yake mapema siku hii yao huku baadhi ya mashabiki wengi wakitafsiri ujumbe huo huenda ndoa yao ikawa imefika mwishoni.

Msanii Alikiba na Aileen Alora wamebahatika kupata watoto wawili tangu walipofunga ndoa mwaka 2018.