Timu ya P Square
Taarifa hii ambayo bado haijathibitishwa rasmi, inachochewa na tamko la kaka na meneja wa kundi la P Square, Jude Okoye kuwa baada ya miaka 10, anaona sasa inatosha, kauli ambayo inahusishwa na taarifa za jamaa huyu kujiondoa katika nafasi yake kama msimamizi wa kundi hili.
Bado hakujatolewa tamko rasmi kwa mashabiki wa kundi hili ambao wameanza kuchanganywa na taarifa hizi huku upande mwingine wa shilingi ukionesha dhahiri kuwa mambo yote yanayoendelea kwa sasa kuhusiana na kundi hili ni mpango rasmi ulioundwa kwaajili ya kuwaandaa watu kwa ujio wa kitu kipya kutoka kwao.