
Ben Pol ambaye hutumia mitandao ya kijamii kuelimisha umma, ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kuwataka wakimaliza kupiga kura warudi nyumbani kusubiri matokeo.
"Kupitia mitandao ya kijamii, mara kadhaa nimekuwa nikiwaambia watu kwamba tufanye uamuzi sahihi, hakuna haja ya kukaa kwenye vijiwe, kupondana kuongea vitu negative, hayo mambo ndio yanaletaga mambo ya uchochezi", alisema Ben Pol.
Ben Pol aliendelea kwa kuwataka wananchi kufanya maamuzi sahihi, na kusimamia katika kile anachoamini.
"Kikubwa ni kwamba mtu unachokishabikia unachokisimamia, kichuje vizuri then ufanye maamuzi yanayotakiwa, piga zako kura then rudi nyumbani upumzike", alisema Ben Pol.