Jumamosi , 26th Sep , 2015

Star wa muziki Tundaman, ametolea ufafanuzi uvumi unaoendelea kusambaa mtaani kuwa yeye na mpenzi wake wanatarajia mtoto, chanzo kikiwa ni kuchanganywa na mkakati wake wa kutangaza rekodi mpya kutoka kwake ambayo itafahamika kwa jina Mama Kija.

Tunda Man

Star huyo ameiambia eNewz kuwa amekuwa akipokea hongera nyingi mtandaoni toka alipoanza kuizungumzia Mama Kija, hii ikiwa ni kazi ambayo inabeba kisa cha kweli kabisa kuhusiana na historia ya maisha yake.