Msanii Tundaman na akiwa na pochi ya mke wake
Tundaman ametokelezea na pochi hiyo kwenye show ya Friday Night Live ya East Africa TV na East Africa Radio ambayo inaruka kila siku ya Ijumaa kuanzia 3:00 mpaka 5:00 Usiku pia huwa Live Facebook na YouTube ya East Africa TV.
"Mke wangu ndio huwa anajua kwamba kabla sijatoka natakiwa nivae nini ili niwe sawa ananisimamia kwenye upande wa mavazi, nimetoka na hii pochi kwa sababu simu yangu kubwa na mfukoni haikai, nimeikuta sehemu yake anayoweka pochi nikakichukua kukivaa na hajui kama nimekichukua" ameeleza Tundaman
Zaidi mtazame hapa chini kwenye video.


