Jumapili , 4th Aug , 2019

Captain wa muziki wa Bongo Fleva Tundaman, kupitia "FNL" ya East Africa Television amemtambulisha mke wake na ameeleza sababu zilimfanya kumnunulia gari.

Tundaman ameeleza hayo baada ya kusambaa kwa video mitandaoni ikionyesha amemzawadia gari mke wake, kwenye kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Kitu nilichokifanya ni kwa sababu ya mke wangu, nimemuonnesha jinsi gani ninavyomjali,amenizalia mtoto sijampa zawadi yoyote kubwa, ambayo nahisi leo au kesho tukiachana aseme kweli kuna zawadi amepewa na mume wangu ambayo imenifikisha sehemu” amesema Tundaman

Aidha Tundaman ametambulisha jina la mke wake huyo aitwaye Sabra Islam au “Mama Intisal” ambaye ni mwanamke wa kiarabu mwenye asili ya Mkoa wa Morogoro.