Ijumaa , 27th Mei , 2016

Msanii mkongwe wa bongo fleva ambae kwa sasa ameamua kujiingiza katika muziki wa injili pia Stara Thomas amewataka wasanii na mashabiki kumuenzi rapper Albert Mangwea.

Msanii wa Bongo fleva na gospo Stara Thomas

Akizungumzan na Enewz Stara amesema kuwa katika kipindi hiki kuelekea katika kukumbu ya kifo cha rapper huyo, tumuenzi kwa yale mema aliyoyafanya huku akiwalaumu vijana wengi na wasanii kuona suala la madawa ya kulevya kama fasheni

Pia Stara alisema kuwa kwa sasa yupo njiani kuachia nyimbo yake ya dini na ya bongo fleva pia, kwani yeye anafanya miziki yote miwili kwa wakati mmoja hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula kusubili ngoma hizo.

Albert Mangwea