Alhamisi , 10th Apr , 2014

Tukio la mwaka 2010 lililohusisha kujeruhiwa kwa risasi kwa msanii Bebe Cool wa Uganda, limechukua sura mpya baada ya askari polisi wa nchini humo, David Oluka ambaye naye alijeruhiwa kwa risasi siku hiyo kudai kuhujumiwa na kupoteza kazi yake.

Bebe Cool

Madai ya askari huyu yanakuja ikiwa ni wiki kadhaa tangu Msanii Bebe Cool kukubaliwa kulipwa fidia ya shilingi milioni 380 za Uganda kutokana na tukio hilo, wakati askari huyu akiambulia barua ya kufukuzwa kazi, akidai kugharamia matibabu kwa kuuza baadhi ya mali za familia.

Katika kuliweka sawa suala hili, Msemaji wa Jeshi la Polisi Uganda amesema kuwa Oluka alipatia stahili zote za matibabu yake na utendaji wake ulidorora huku akijipatia likizo bila taarifa kwa kisingizio cha tukio hili huku akiwa anatarajia kulipwa fidia kitu ambacho si sawa.