
Kushoto ni muigizaji Duma na kulia ni mwongozaji wa filamu Timoth
Akizungumza na eNEWZ, Daudi Duma, amekanusha vikali kauli ya Timoth na kusema kuwa amezoea kutengeneza filamu za kutisha na yeye (Duma) amezoea kuigiza filamu zenye stori ambazo kwake Timoth haziwezi.
"Mimi siwezi kubishana na Timoth kwa sababu yeye anafanya filamu za kutisha na mimi nafanya filamu za 'love story' hivyo ni vitu viwili tofauti. Mimi ndio msanii pekee ambaye nimeweza kujaza watu Mlimani City kwenye uzinduzi na hadi Waziri alihudhuria yeye ni nani aseme filamu ni mbaya?'', amehoji Duma.
Pia ameongeza kuwa kuna filamu ambazo tayari zilishatoka huko nyuma kwa nini asingeongea amekuja kuongea baada ya filamu ya kutoka huku akidai kuwa amekuwa akijitahidi kwenda mpaka Kenya ili tu kufikisha soko la filamu nje ya nchi.
Duma hivi karibuni alizindua filamu yake inayokwenda kwa jina la 'Nipe Changu' ambapo uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Naibu Waziri Wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo Juliana Shonza, wasanii na wadau mbalimbali.