Jumatatu , 19th Jan , 2015

Tamasha kubwa kabisa la muziki la aina yake lijulikanalo la "Tigo Kiboko Yao” linatarajiwa kutikisa ardhi ya jiji la Dar Jumamosi hii Januari 24, mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, burudani ambayo itaanza saa 8 mchana.

Msanii wa kizazi kipya Saraha Kaisi a.k.a Shaa

Baadhi ya wasanii kiboko yao 18, watakaopanda jukwaani katika tamasha hilo ni pamoja na Weusi, AY, Mwana Fa, Fid Q, Profesa Jay, Shaa,Vanessa Mdee, Jux, Ben Pol, Linah, Shilole, Isha Mashauzi, Khadija Kopa, Sikinde Band, Msondo Band, Yamoto band, Christian Bella akiwa na Malaika Band, Ali Kiba na Diamond Platnumz.

Njia ya kujipatia tiketi ya kushuhudia tamasha hili ni kununua kifurushi cha wiki ama mwezi kwa simu yako kwa kutumia line ya Tigo, kisha utatumiwa ujumbe kukujulisha kama umefanikiwa kupata nafasi ya kwenda kushuhudia onesho hili, ujumbe ambao utaujibu kwa kutuma neno 'Kiboko Yao' kukuwezesha kutumiwa Code namba ambayo ndiyo itakuwa tiketi yako.

Usikose kuja kushuhudia burudani hii ya kihistoria na kumbuka, tiketi 6,000 zitakuwa zikitoka kila siku, hivyo ujanja ni kuwahi kununua kifurushi mapema. Tigo Kiboko Yao.