Alhamisi , 15th Feb , 2018

Msanii wa filamu nchini Tanzania na Rais wa watoto, Tausi Mdegela amefunguka na 'kuwachamba' watu wanaomsema vibaya kuhusiana na mavazi yake anayovaa na kudai kama inawakera basi wakanunue nguo wampelekee na sio kumpangia cha kuvaa.

Tausi ametoa kauli hiyo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kwenye ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa 10 alasiri baada ya baadhi mashabiki zake wakimshambulia kuhusu nguo zake katika mitandao ya kijamii. 

"Mimi ni Tausi na nitabaki kuwa Tausi tuu, nivae joho, pensi hata taiti ni mimi tu. Kwa hiyo mtu hawezi kunipangia maamuzi kuhusu mavazi eti usivae hichi vaa kile. Niletee dera halafu chukua zile pensi choma 'simple' tu", amesema Tausi.

Pamoja na hayo, Tausi ameendelea kwa kusema "kwa sababu mimi nimenunua hiyo pensi yangu ni hela ambayo niliyokuwa nayo hiyo siku nikaona nisiondoke mikono mitupu nikanunua hiyo pensi. Wewe ambaye inakukwaza niletee nguo ambayo unahisi nitapendeza tofauti na ninavyovaa".

Kwa upande mwingine, Tausi amedai kama mpenzi wake akimsifia kuwa amependeza kutokana na mavazi aliyoyavaa hawezi kumpa nafasi mtu mwingine kumsikiliza juu ya alichokivaa.

Lipa kwa M-PESA sasa na upate zawadi na punguzo katika sehemu mbalimbali za huduma kwa kubonyeza *150*00# au MENYU ya mtandao uliopo, VODACOM, PESA NI M-PESA.