Jumatano , 2nd Dec , 2015

Muigizaji ambaye sasa hivi amekuwa gumzo kupitia filamu ya Empire Taraji P. Henson, ameungana na msanii Alicia Keys katika mpango wa kusaidia watoto wanaoishi na virusi vya UKIMWI barani Afrika.

Taarifa hiyo ya muigizaji Taraji na wenzake imetolewa siku ya jumanne ambayo ndio ilikuwa siku ya UKIMWI duniani, ambapo Taraji Henson, mwanamuziki Janelle Monae pamoja na Laila Ali ambaye ni mtoto wa bondia maarufu Mohamed Ali, wamesainiwa kama mabalozi wa mpango huo ambao Alicia Keys ameuanzisha kwa lengo la kusaidia watoto wanaoishi na virusi vya unaoitwa “keep a child alive”

“UKIMWI ni ugonjwa namba moja unaosababisha vifo vya vijana katika nchi za jangwa la sahara, na namba mbili katika kusababisha vifo duniani, nina heshima kuunga mkono Keep a child alive katika kupambana kumaliza ugonjwa huu”, alisema Taraji.

Nae mwanamuziki Monae aliongeza kwa kusema kuwa “tunahitaji kuungana na kutumia sauti zetu na kumaliza maambukizi haya”.

Mwezi uliopita Alicia Keys alifanya tukio la kuchangia pesa jijini New York na kufanikiwa kupata dola milioni 3.8, ambapo mchekeshaji maarufu Chriss rock ndiye alikuwa mshereheshaji wa tukio hilo.

Alicia keys ameanzisha mpango huo wa kusaidia watoto wanaoishi na virusi vya UKIMWI barani Afrika mwaka 2003, na tayari mpaka sasa ameshasaidia baadhi ya watoto wanaoishi nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, South Africa na India.

Taraji Henson akiwa na Alicia Keys
Laila Ali ambaye ni mtoto wa Bondia Mohamed Ali.