Swali la AY kwa wasanii wa sasa

Jumanne , 8th Jun , 2021

Legendary wa muziki na mfanyabiashara AY  amesema wakati anaenda kwenye tuzo za MTV alikuwa anabeba nyimbo za wasanii wengine kwa ajili ya kupata nafasi ya kupenya huko, pia  ameuliza wasanii wa sasa kwamba wanaweza kufanya jambo hilo.

Msanii AY kwenye studio ya East Africa Radio

AY ameelezea hilo kupitia kipindi cha Supa Breakfast 'Menu Mpya' ya East Africa Radio, kwa kusema wasanii wa sasa wawe na upendo kwani  hawezi jua kesho atakuwa wapi na atasaidiwa na nani.

"Zamani ulikuwa unapambana peke yako, mimi niliona sio sawa kusafiri peke yangu nikawa nabeba nyimbo za wasanii wenzangu kuwapelekea MTV, swali langu hawa wa sasa hivi wanaweza kufanya hivyo, nilikuwa nachukua hadi nyimbo za Kenya ili kupigwa MTV"

"Dawa ni kusambaza upendo tu, lazima tupendane haya maisha yapo tu, leo unaweza ukamfanyia mtu hivi kesho unamkuta yeye ndio boss you never know, video ya habari ndio hiyo au ngoja ageuke tulichukua mastaa kibao, hiyo ndio love"

"Napenda kuishi nikiwa Neutral sifungamani na chochote, Memory ambayo nikisema nimebugi sikumbuki japo nilikuwa napigwa vita ya chinichini, kwenye maisha hatuwezi kufanana kuanzia kwenye mpira, muziki au hata kwa madaktari" ameongeza