Msanii Stamina
Stamina amefunguka hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio alipokuja kutambulisha ngoma yake mpya aliyowashirikisha rapa mkongwe Prof Jay pamoja na One Six.
''Ninatoa Album hivi karibuni na itakuwa na nyimbo 8 japo jumla zitakuwa 10 ukijumlisha na Intro pamoja na Outro'', amesema.
Pia ametoa shavu kwa Prof Jay juu ya uwezo alioonesha kwenye ngoma ya BABA. ''Imekuwa poa sana kufanya kazi na brother, ambaye kwenye ngoma yetu ya #BABA amekuwa baba kweli na mapokezi ya wimbo yamekuwa makubwa, naamini kazi bora zitaendelea''.
Prof Jay pamoja na Stamina
Moja ya ngoma ambazo Stamina amesema zitakuwepo kwenye album hiyo ambayo haweka wazi ni lini haswa itatoka ni pamoja na Nalewa leo aliyomshirikisha Maua Sama na Asiwaze.