Jumamosi , 19th Sep , 2015

Stamina, mwana hip hop ambaye amekuwa na msimamo mkali katika mtindo wake wa kuchana na vilevile uandishi wa mistari, ametoa maneno mazito kwa wasanii wa rap ambao huandikiwa mistari na pia kujisifu katika kubadilisha aina ya flows yani ku-switch.

Stamina a.k.a Shorwebwenzi

Stamina ameweka bayana msimamo wake huo, akitolea mfano marapa wakongwe akiwepo Proffesa Jay, Jay Moe na Solo Thang, binafsi akiwa hana imani na uandishi wa marapa wengi wanaofanya muziki hapa Bongo.