Ijumaa , 23rd Mei , 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania, Snura Mushi amesema kuwa, kutokana na majanga ya kimaadili yaliyomkuta, kwa sasa yupo katika utayarishaji wa video yake mpya ya Ushaharibu, akiwa makini kabisa kuzingatia vigezo vya maadili.

Snura Mushi jukwaani

Snura ambaye anakiri kuwa video yake ya Nimevurugwa imempotezea nafasi nyingi sana alizokuwa anatarajia kutoka nayo, amesema kuwa amejifunza kutokana na makosa, na kwa wale wapenzi wa Viuno, Mwanadada huyu amesema katika kazi hii amewawekea kwa kipimo.

Hapa Snura anafunguka mwenyewe juu ya video hii ambayo anafanya chini ya muongozaji video Adam Juma.