Ijumaa , 18th Dec , 2015

Msanii wa muziki Snura ambaye misingi ya kile anachokifanya imejengeka kutoka katika tasnia ya uigizaji ametoa maoni yake kuwa, tasnia ya filamu inaweza kuamishwa tena kwa kuhusisha visa kutoka rekodi za muziki ambazo zimefanya vizuri.

Msanii wa muziki nchini Snura

Snura ametolea mfano wa rekodi yake ya Majanga ambayo anaamini kama ataifanyia filamu, itajenga hamu kubwa ya mashabiki kuitazama na kuamsha mvuto wa soko la kazi hizo ambalo linaonekana kudorora kwa sasa kama ambavyo anaeleza hapa.