Jumatatu , 19th Feb , 2018

Msanii wa muziki bongo fleva Juma Jux amefunguka na kudai heshima aliyopewa nchini Burundi hakuna mwana muziki yeyote aliyowahi kupewa ya kuimbiwa wimbo wa taifa wa nchi hiyo kwenye show.

Jux amebainisha hayo kupitia ukurasa wake maalum wa kijamii mara baada ya kumaliza 'show' yake katika fukwe za bahari ya Lacost nchini humo mwishoni mwa juma lililopita.

"Asanteni sana burundi sitaweza kuja kusahau upendo wenu kwenye maisha yangu japo mvua kubwa kunyesha bado mkakubali mnyeshewe nakuja kwa wingi sana kwenye 'show'. 'We made a history' nashukuru kwa heshima yenu ya kuniimbia wimbo wa taifa kama heshima yenu kwangu na hii haijawahi kutokea kwa msanii yoyote aliyewahi kuja burundi", amesema Jux.

Kwa upande mwingine, Jux ni miongoni mwa wasanii wanaotegemewa kuachia albumu hivi karibuni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mpenzi wake Vanessa Mdee.