Mama Asha Baraka baada ya kusikia kauli hiyo amesema anamshangaa sana Ali Choki kusema maneno hayo kwani tangu mwaka jana alishamruhusu akafanye kitu anachotaka hata kama ikiwa ni pamoja na kazi zake binafsi.
''Namshangaa sana Ali Choki mimi nishampa ruhusa afanye kazi nyingine yoyote bila kujali mkataba wetu unasemaje hivyo yeye aendelee na mambo yake wala asinifikirie'' amesema.
Asha Baraka pia amesema kuwa hataki Ali Choki afie Twanga Pepeta hivyo kama ana uwezo arudi akaifufue Extra Band kwani alimpa uongozi ndani ya Twanga Pepeta akashindwa kuiongoza.
Ali Choki tayari ameshaonekana akiingia studio na msanii Beka Flavour kuandaa kazi zake binafsi hivyo huenda akawa tayari ameshajiandaa na maisha bila ya Twanga Pepeta. Zaidi tazama eNEWZ ya EATV.
