Nedy Music ndani ya FNL
Nedy ametoa msimamo huo bila kueleza kwa kina sababu ya maamuzi hayo, alipokuwa katika kipindi cha FNL cha EATV baada ya kuenea kwa taarifa kuwa kuna collabo kati yake na msanii mmoja wapo kutoka Wasafi.
Nedy ambaye ametoa ngoma yake ya pili chini ya PKP aliyoko pia Ommy Dimpoz, amesema taarifa hizo siyo za kweli na kwamba hana ugomvi wowote Wasafi, isipokuwa kinachoendelea ni masuala ya kazi tu.
Kuhusu yeye kusalimiana na Wasafi amesema hana kinyongo na akikutana nao mahali popote atawasalimia "Nikikutana na Msafi (msanii kutoka Wasafi) yoyote nitamsalimia kama kawaida kama washkaji, lakini kama yeye hataonesha ushirikiano basi salamu itakuwa haina haja"