Jumamosi , 5th Dec , 2015

Rapa Baghdad ameahidi kuweka bayana mambo mengi ambayo mashabiki wana kiu ya kufahamu juu yake, kupitia Documentary ambayo amejipanga kuachia tarehe 11 mwezi wa 2 mwaka ujao.

baghdad na mkewe Gift

Baghdad ambaye amepitia hatua kadhaa za mabadiliko kwa upande wa sanaa yake na hata maisha binafsi, akiwa sasa ni baba wa familia mwenye mtoto mmoja (Kyle), amesema baadhi ya mambo ambayo yatahusika katika Documentary hii ni pamoja na tuhuma za yeye kuitwa shoga, kugombana na kuchukuliwa mpenzi na producer na msanii Mesen Selekta, kuibuka na kupotea kwa kundi la Mexicana Lacavela kati ya ishu nyingine kibao.

Msanii huyo amesema kuwa, mpango huo mzima sambamba na mafanikio ambayo ameanza kuyapata kijamii na kiuchumi, vitakuwa katika documentary hiyo ambayo tarehe aliyochagua kuitoa itakuwa pia ni siku ya maadhimisho ama kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.