Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

"Sikuwa nimejipanga"- Linah

Jumamosi , 16th Sep , 2017

Msanii wa bongo fleva, Linah Sanga amefunguka na kudai hakuwa amejipanga kwa kipindi hiki kuwa na mtoto ila anamuomba Mungu isiwe kigezo cha yeye kupotea katika muziki ili aje kuwa mfano kwa wasanii wenzake wa kike wanaogopa kubebea ujauzito.

Msanii wa bongo fleva, Linah Sanga.

Linah amebainisha hayo kupitia kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE 'FNL' kutoka EATV baada ya kuwepo imani kwa baadhi ya watu wakidai msanii akioa, akiolewa hata akijifungua na mtoto mara nyingi hawezi kuendelea kufanya vizuri katika kazi zake kwa kuwa majukumu ya ulezi yanaongezeka na kupelekea kupotea katika 'industrial' ya muziki.

"Nina muomba Mungu usiku na mchana nisije kupotea katika 'game' kwa sababu ya uzazi, ili iwe mfano hata kwa wengine ambao watakuja nyuma yangu, labda wanaogopa kuzaa kwa kufikiri watapotea. Ila mimi nafikiri ni jinsi mtu mwenyewe anavyoishi na mashabiki zake", amesema Linah.

Pamoja na hayo, Linah ameendelea kwa kusema "Sikuwa nimejipanga kupata mtoto katika kipindi hiki ila nilikuwa na-wish nipate ujauzito nizae lakini sikufahamu ni lini itanitokea hivyo. 'So' kipindi kile nilichokuwa na-wish nikawa kila nikijaribu haingii, nikajisahau na kujikuta imekuja hata sikutarajia, lakini kwa kuwa nilikuwa nina uhitaji nikasema hakuna neno. Japo nilishauriwa vitu vingi sana mwanzoni lakini nikasema hapana kwa kuwa nimetaka kuzaa acha nifanye hivyo", amesisitiza Linah.

Kwa upande mwingine, Linah amesema kwa anajipa mapumziko katika kufanya kazi zake na kuwataka mashabiki zake wamvumilie mpaka mwakani (2018) katika miezi ya mwanzoni ndipo atakapoachia kazi yake mpya.

HABARI ZAIDI

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu