M-rap
Msanii anayekuja kwa kasi katika tasinia ya Bongo fleva M-rap ambaye kwa sasa ana ngoma yake mpya kamshilikisha Young D inayoitwa unazungumzia nini amekutana na Camera ya Enewz na kupiga stori mbili tatu
Hata hivyo M-rapa alifunguka kuhusiana na mahusiano yake ya kimapenzi na kusema ana mpenzi wake ambaye anatokea Zanzibar na huwa anaishi naye kwa hiyo watu wabaki tu muziki wake lakini wa upande wa mahusiano tayari yupo na mtu.
M-rap amemalizia kwa kusema watu wanao msema kuwa geto lake analokaa sinza amepangishiwa na mwanadada wake huyo sio kweli kwa kuwa geto hilo kapangisha kwa pesa yake mwenyewe ambayo anaipata akifanya show.
Pia amemalizia kwa kusema imezoeleka wanamuziki wengi wanaorap wanaishia katika madawa ya kulevia lakini kwake ni tofauti kwani huwa mama yake anamsihi kila mara na pia yupo shule anasoma hivyo anazidi kupata uelewa wa maisha zaidi.





.jpg?itok=5cvL0YaP)