Jumanne , 31st Oct , 2023

Mwanamuziki kutoka Nigeria Rema ametumbuiza kwenye usiku wa kihistoria wa utoaji wa Tuzo za Ballon d'or ambazo zimefanyika jijini Paris Ufaransa usiku wa kuamkia leo na kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa Afrika kutumbuiza kwenye hafla hiyo.

Picha ya Rema

Kwenye hafla hiyo mshambuliaji wa Argentina na Inter Miami, Lionel Messi, alitangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Ballon d’Or 2023 kwa mara ya nane baada ya kusaidia Taifa lake kushinda Kombe la Dunia nchini Qatar, mwaka jana.

Rema aliimba wimbo wake unaopendwa na wengi duniani "Calm Down" na wenye historia kubwa kwenye safari yake ya muziki  kwa kushinda tuzo nyingi zaidi Tuzo kama MTV (Best Afrobeats ) Trace Awards  (Song of the year)  The Headies (Best Music Video) na nyingine kibao.